Timu kuwasili nyumbani Alfajiri

Kikosi chetu kimeanza safari ya kurejea jijini Dar es Salaam kutoka Misri na kinatarajia kuwasili saa 10 Alfajiri.

Baada ya kufika kikosi kitaingia kambini moja kwa moja kuanza maandalizi ya mchezo wa hatua ya 16 bora ya CRDB Bank Federation Cup dhidi ya Mashujaa FC.

Mchezo huo utapigwa Jumanne ya Aprili 9 saa 10 jioni katika Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma na tunahitaji kushinda ili kutinga robo fainali.

Tunajua Mashujaa wapo kwenye kiwango bora na wana timu imara hasa wakiwa Uwanja wa nyumbani lakini tumejiandaa kuhakikisha tunashinda.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER