Kikosi chetu kitaondoka saa saba mchana kuelekea mkoani Lindi tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Namungo utakaopigwa Jumatano saa moja usiku katika Uwanja wa Majaliwa
Kikosi kinatarajia kufika Lindi usiku ambapo wachezaji watapata mapumziko na kesho watafanya mazoezi ya mwisho kujiweka sawa kabla ya kushuka dimbani Jumatano.
Baada ya mchezo wa Jumatano kikosi kitabaki huko huko Lindi kujiandiaa na mchezo wa nusu fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Azam FC utakaopigwa mwishoni mwa wiki.