Kikosi chetu kitaondoka leo mchana kuelekea mkoani Morogoro tayari kwa mchezo ujao wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa Jumamosi Uwanja wa Manungu.
Kabla ya kuondoka kikosi kilifanya mazoezi katika viwanja vyetu vya Mo Simba Arena ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo huo.
Wachezaji wetu wawili Jonas Mkude na Kibu Denis hawatakuwa sehemu ya kikosi kutokana na kuendelea kuuguza maumivu waliyopata katika mchezo uliopita dhidi ya Mbeya City.