Timu kuondoka kesho kuelekea Afrika Kusini

Kikosi cha wachezaji 23 kitaondoka kesho asubuhi kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stellenbosch utakaopigwa Jumapili ijayo.

Kikosi kitaondoka na Ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) ambapo itapitia Johannesburg kabla ya kuunganisha kuelekea Durban ambapo ndipo kutakapopigwa mchezo huo.

Baada ya kikosi kufika Afrika Kusini kesho jioni kitafanya mazoezi ya Gym ili kuweka miili sawa kutokana na uchovu wa safari.

Timu inaondoka ikiwa na matumaini ya kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika licha ya ugumu ambao tunategemea kukutana nao.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER