Kikosi chetu kitaondoka kesho asubuhi kuelekea mkoani Kagera tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya wenyeji Kagera Sugar utakaopigwa Jumatano Uwanja wa Kaitaba.
Tunatarajia kuondoka na kikosi kamili kwa ajili ya mchezo huo ambao tumeupa umuhimu mkubwa ambao tunahitaji kupata alama tatu muhimu.
Licha ya kutopata ushindi katika mechi mbili zilizopita morali ya wachezaji ipo juu na wameahidi kujitoa kwa timu ili kuhakikisha tunapata ushindi.
Wachezaji wamefanya mazoezi ya jioni jijini Dar es Salaam leo na kesho tunatarajia tukifika Kagera tutafanya ya mwisho katika Uwanja wa Kaitaba kabla ya kushuka dimbani Jumatano saa 10 jioni