Kiungo wetu mkabaji Taddeo Lwanga amechaguliwa mchezaji bora wa Uganda kwa mwaka 2021 kutokana na ubora aliounyesha msimu ulipoita.
Msimu uliopita Taddeo alicheza mechi nyingi na amekuwa mhimili wa timu katikati ya uwanja akiwalinda vema mabeki watatu.
Lwanga amebeba Tuzo hiyo baada ya kuwashinda Eric Kambale na Yunus Sentamu.
Katika kura 1,124,568 zilizopigwa, Lwanga amepata kura 468, 631, Kambale alishika nafasi ya pili kwa kura 399,426 na Ssentamu aliyepata kura 256,529 alishika nafasi ya tatu.
Taddeo amesema ni heshima kubwa kwake kupata tuzo hiyo na amewashukuru mashabiki kwa kumpigia kura na ameahidi kuendelea kupambana ili kulipa furaha.
“Kwangu ni heshima kubwa kupata tuzo hii, inazidi kunifanya niendelee kupambana ili kuwapa furaha mashabiki ambao wamenipigia kura nyingi na hilo ndilo nawaahidi,” amesema Taddeo.