Taddeo aeleza furaha ya kufunga kwenye michuano mikubwa

Kiungo mkabaji Taddeo Lwanga, ameweka wazi furaha yake ya kufunga bao muhimu kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana mchezo uliopigwa jana.

Taddeo alifunga bao hilo dakika ya pili baada ya walinzi wa Jwaneng kuzembea kuondoa mpira wa kona uliopigwa na kiungo Rally Bwalya.

Kiungo huyo raia wa Uganda amesema anaamini ataendelea kufunga na kuisaidia Simba kupata matokeo endapo atapata nafasi ya kufanya hivyo.

“Kama mchezaji najisikia furaha kufunga kwenye michuano mikubwa kama hii na kuisaidia timu kupata ushindi ugenini, binafsi naamini nitaendelea kufunga kama nikipata nafasi,” amesema Taddeo.

Kicha ya kuwa na mtaji mzuri wa mabao mawili ya ugenini Taddeo amesema bado hatutakiwi kuwachukulia poa Galaxy katika mchezo wa marudiano wiki ijayo kwani wana timu nzuri na kwenye soka lolote linawezekana.

“Galaxy siyo timu mbaya, wako vizuri bado tunapaswa kuhakikisha tunachukua tahadhari ili kupata ushindi wiki ijayo na kufuzu hatua ya makundi na hilo ndilo lengo letu,” amesema Taddeo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER