Bodi ya Ligi Kuu Tanzania TPLB imeahirisha mchezo wetu dhidi ya Dodoma Jiji ambao ulipangwa kuchezwa Jumamosi, Februari 15 katika Uwanja wa KMC Complex.
Sababu ya kuahirishwa mchezo huo ni kutokana na wachezaji wa Dodoma Jiji kupata ajali katika Wilaya ya Ruangwa wikiendi iliyopita.
Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi inasema Maafisa na baadhi ya wachezaji hawapo sawa kiafya hivyo hawataweza kuwa sehemu ya mchezo hivyo mechi imeahirishwa.
TPLB imesema itatoa taarifa muda si mrefu ya lini mchezo huo utapigwa tena.