Uongozi wa klabu ya Simba unautaarifu Umma kuwa Kocha Juma Ramadhani Mgunda hatokuwa sehemu ya benchi la ufundi la Simba Queens baada ya mkataba wake kutamatika.
Uongozi wa Simba unapenda kumshukuru Mwalimu Mgunda kwa utumishi wake ndani ya klabu yetu akianza kukitumikia kikosi cha Simba cha Wanaume ( Simba Senior Team) kisha kuhamishiwa timu ya Wanawake (Simba Queens) na kote akitimiza vema majukumu yake.
Ndani ya kipindi cha mwaka mmoja Mwalimu Mgunda ameiwezesha Simba Queens kurejesha taji lake la ligi kuu ya Wanawake Tanzania (TWPL).
Kwa sasa Simba Queens itakua chini ya Kocha msaidizi, Mussa Hassan Mgosi ambae tayari ameshaanza maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu ambayo itaanza hivi karibuni.