Uongozi wa Klabu umefikia makubaliano ya pande zote ya kuvunja mkataba na kocha mkuu, Pablo Franco Martin baada ya kutofikia matarajio yaliyokuwa yamewekwa.
Katika kipindi chake Pablo ametuwezesha kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi na kufika Robo Fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika.
Uongozi una mshukuru Pablo kwa mchango wake mkubwa ndani ya timu ambapo baada ya kuondoka kikosi kitakuwa chini ya Kocha Msaidizi, Selemani Matola.
Wakati huo huo tumefikia makubaliano ya pande zote ya kuvunja mkataba na kocha wa viungo, Daniel De Castro Reyes.
Simba inawatakia kila kheri kocha Pablo na mtaalam wa viungo Daniel Castro katika majukumu yao mapya.
Simba Nguvu Moja.
Barbara Gonzalez
Afisa Mtendaji Mkuu
Simba Sports Club
31 May 2022