Preview

Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) imeahirisha mchezo wetu dhidi ya Mtibwa Sugar ambao ulipangwa kuchezwa Jumapili ya Februari 18 katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

Sababu ya kuahirishwa kwa mchezo huo ni kutupa nafasi ya kusafiri hadi nchini Ivory Coast kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas utakaopigwa Ijumaa, Februari 23.

Bodi ya Ligi imeona kama tungecheza mchezo dhidi ya Mtibwa tusingepata muda wa kujiandaa na mechi ya ASEC huku ikizingatiwa tunapaswa kusafiri umbali mrefu.

Mchezo wetu ulioahirishwa dhidi ya Mtibwa utapangiwa tarehe nyingine ya kuchezwa.

Details

Date Time Full Time
February 16, 2024 1:58 pm 90'