Sita waitwa Taifa Stars kufuzu Kombe la Dunia

Nyota wetu sita wameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kujiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Morocco.

Mchezo huo ambao utakuwa ni wa marudiano utapigwa nchini Morocco, Machi 26 kufuatia ile ya kwanza iliyopigwa jijini Dar es Salaam, Novemba 21, 2023 na Stars kupoteza kwa mabao 2-0.

Nyota hao ni mlinda mlango Ally Salim, walinzi Shomari Kapombe, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ na Abdulrazak Hamza.

Wengine walioitwa ni pamoja na viungo Yusuph Kagoma na Kibu Denis.

Taifa Stars itaingia kambini kesho kujiandaa na mchezo huo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER