Kikosi chetu kimeendelea na mazoezi katika Uwanja wa Boko Veterans kujiandaa na mchezo wa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana.
Mchezo huo wa mkondo wa kwanza utapigwa Jumapili, Oktoba 17 katika Uwanja wa Taifa wa Botswana saa 10 jioni kwa saa za nyumbani.
Morali za wachezaji zipo juu huku kila mmoja akionekana kufanya jitihada kulishawishi benchi la ufundi ili kumpa nafasi katika mchezo huo.
Timu inafanya maandalizi ya mwisho mwisho kabla ya kuanza safari ya kuelekea Botswana tayari kwa mchezo huo.
Tumejipanga kuhakikisha tunafanya vizuri katika mchezo wa Jumapili ili mechi ya marudiano nyumbani isiwe na presha kwetu.