Kikosi chetu kimewasili salama jijini Mwanza leo kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa Uwanja wa CCM Kirumba Alhamisi Juni 3, mwaka huu.
Timu imeondoka na jumla ya wachezaji 20 ambapo jioni itafanya mazoezi ya kuweka miili sawa tayari kwa mchezo huo.
Mchezo huo ni wa kiporo ambapo ulisogezwa mbele kutokana na ushiriki wetu wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Tunaingia kwenye mchezo dhidi ya Ruvu tukiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Namungo tuliopata Jumamosi iliyopita.
Kuelekea ukingoni mwa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2020/21 tumejiandaa kuhakikisha tunashinda mechi zote nane zilizobaki ili kutetea ubingwa wetu kwa mara ya nne mfululizo.
2 Responses
AWALI YA YOTE NAHIPONGEZA SANA TIMU YANGU KWA KUENDELEA KUFANYA VIZURI NA BEACH ZIMA LA UFUNDI.NAHOMBA UONGOZI MSHIKAMANO MLIO NAO MUENDELEZE HIVYO NDIO SIRAHA YETU WANA SIMBA. PILI KUANGALIA UWEZEKANO WA BEACH ZIMA LA UFUNDI KULIONGEZEA MIKATABA YAO KWANI JITIHADA ZAO TUNAZIONA.
SIMBA is another level… May God bless SIMBA