Simba yarejea mazoezini leo

Baada ya mapumziko ya siku mbili kikosi chetu kinarejea mazoezini leo kujiandaa na mchezo wa hatua ya kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwnaneng Galaxy ya Botswana.

Mchezo huo utapigwa Oktoba 17 nchini Botswana na utakuwa wa kwanza kwetu baada ya kupisha mechi za Timu ya Taifa.

Wachezaji watakaoanza mazoezi leo ni wale ambao hawajaitwa kwenye timu zao za taifa huku wale walioitwa wakiruhusiwa kwenda kujiunga na wenzao.

Nyota wetu 16 wameitwa kwenye timu zao za taifa ambapo tisa wamejumuishwa Taifa Stars wakati saba ni wale wa kimataifa ambao wameitwa na mataifa yao.

Baada ya majukumu ya timu za taifa wachezaji watarejea haraka kikosini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wetu wa Ligi ya Mabingwa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER