Simba yapiga mazoezi ya lala salama kuivaa Namungo

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho leo jioni kwenye Uwanja wa Majaliwa kujiandaa na mchezo wa kesho dhidi ya Namungo FC.

Katika mazoezi ya leo jioni wachezaji wote wameshiriki ambapo hakuna hata mmoja miongoni wa 20 waliopo aliyepata maumivu hivyo wote wako tayari kwa mchezo.

Mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara utaanza saa 10 jioni katika Uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi.

Katika msimu huu, Namungo ndiyo timu pekee ambayo hatujacheza nayo mechi yoyote ya ligi kutokana na ushiriki wetu wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika huku wao wakishiriki Kombe la Shirikisho.

Kama tutashinda mchezo wa kesho tutafikisha pointi 64 alama tatu juu ya wanaoshika nafasi ya pili huku bado tukiwa na michezo mitatu mkononi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER