Kikosi chetu kimepangwa na Red Arrows kutoka Zambia katika mchezo wa mtoano wa Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Droo ya michuano hiyo imefanyika jijini Cairo nchini Misri mchana huu ambapo timu zote zinatafuta tiketi ya kuingia hatua ya makundi.
Kikosi chetu kitaanzia nyumbani katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Novemba 28 kabla ya mchezo wa marudiano utakaofanyika nchini Zambia, Desemba 5.