Simba, Yanga kukipiga Ngao ya Jamii Septemba 25

Mchezo wa Ngao ya Jamii ya kufungua msimu mpya wa ligi 2021/22 kati yetu na Yanga utapigwa Septemba 25 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetangaza rasmi tarehe hiyo ya mchezo ambapo kwa upande wetu tutahakikisha tunapata ushindi ili kuanza vizuri msimu.

Katika mchezo wa Ngao ya Jamii ya kufungilia Msimu wa 2020/21 dhidi ya Namungo FC uliopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Agosti 30, mwaka jana tuliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Mabao yetu yalifungwa na Nahodha John Bocco na Bernard Morrison kwa mkwaju wa penati.

Endapo tutashinda mchezo huo itakuwa ni mara ya tano mfululizo tangu mwaka 2017, 2018, 2019 na 2020.

SHARE :
Facebook
Twitter

3 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER