Simba, Yanga hakuna mbabe

Mchezo wa hatua ya Nane Bora wa Ligi Kuu ya Vijana Chini ya Umri wa Miaka 20 kati yetu na Yanga uliopigwa Uwanja wa Azam Complex umemalizika kwa sare ya bila kufungana.

Mchezo ulianza kwa kasi huku timu zikishambuliana kwa zamu lakini zilishindwa kuzitumia na kufanya kwenda mapumziko zikiwa hazijafungana.

Dakika ya 28 Nahodha, Andrew Michael alipoteza nafasi ya wazi baada ya mpira aliopiga kugonga mwamba kufuatia kuwapiga chenga walinzi wa Yanga.

Mlinda mlango wetu Ahmed Feruz aliokoa mpira wa adhabu uliokuwa unaelekea nyavuni kwa uhodari mkubwa uliopigwa na mlinzi Said Mashoto sekunde chache kabla ya timu kwenda mapumziko.

Kocha Nico Kiondo alimtoa Andrew Michael ambaye alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia na kumuingiza Kassim Omari.

Washindi wawili kutoka kundi A na B wataingia nusu fainali na wawili wataingia faianali kabla ya kupatikana bingwa.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER