Klabu yetu imeingia mkataba wa miaka miwili na Shirika la Ndege Tanzania (Air Tanzania) kuwa wasafirishaji wetu rasmi wa safari za ndani na nje ya nchi wenye thamani ya zaidi Sh milioni 400.
Mtendaji Mkuu wa klabu, Barabara Gonzalez amesema kabla ya mkataba kulikuwa na mazungumzo ya muda mrefu ambavyo itakuwa na manufaa pande zote.
Barbara amesema kuanzia sasa Air Tanzania ndiyo wasafirishaji rasmi wa timu yetu na tutawatangaza kila tutakupokuwepo.
“Leo tumeingia mkataba na Shirika letu la Ndege kwa ajili ya kutusafirisha katika safari zote ndani na nje kwa muda wa miaka miwili,” amesema Barbara.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Air Tanzania, Ladislaus Matinde amesema wameamua kufanya kazi na timu yetu kutokana ukubwa wa ‘brand’ yetu tulionao.
“Simba ina brand kubwa na tunajua itakuwa ni faida kwetu na kwao pia, Simba itatutangaza kote itakapokuwa nasi pia tutaitangaza, kwa hiyo mkataba huu una faida kwa pande zote,” amesema Matinde.