Kikosi chetu leo kimecheza mechi ya kirafiki ya kimazoezi na kituo cha Cambiaso Sports na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 mchezo uliopigwa Uwanja wa Boko Veterans.
Katika mchezo huo tulifanikiwa kupata mabao matatu kipindi cha kwanza kupitia kwa Pascal Wawa kwa kichwa, Bernard Morrison kwa mpira wa adhabu na Abdul Swamad Kassim kwa shuti kali.
Kipindi cha pili Cambiaso walipata bao moja kwa mkwaju wa penati kabla ya Hassan Dilunga kumalizia la nne akitokea benchi.
Kocha Didier Gomes aliwaingiza Dilunga, Ambokise Mwaipopo na
Samson Lucas kuchukua nafasi za Wawa, Yusuffu Mhilu na Saad Noshard.
Kikosi Kamili kilivyokuwa
Beno Kakolanya (30), Said Noshard,
Gadiel Michael (2), Pascal Wawa (6), Henock Inonga (29), Abdul Swamad Kassim (25) Jimmyson Mwanuke (21), Jonas Mkude (20)
Yusuf Mhilu (27), Ibrahim Ajib (10)
Bernard Morrison (3).