Baada ya kupata ushindi lakini kwa idadi ndogo ya mabao benchi la ufundi limejipanga kuhakikisha tunaanza kutoa dozi tukianza katika mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Coastal Union.
Kocha Msaidizi Seleman Matola, amesema mapungufu yaliyojitokeza katika mechi zilizopita yamefanyiwa kazi na anaamini ushindi mnono utaanza kupatikana.
Matola amesema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na asubuhi wamefanya mazoezi ya mwisho na kila kitu kinaenda sawa kuelekea mechi ya kesho.
“Ni kweli tumekuwa hatupati ushindi mnono lakini tumeyaona mapungufu yetu na tumeyafanyia kazi, matumaini yetu ushindi mnono utaanza kupatikana.
“Coastal ni timu nzuri ina wachezaji wazuri tunawaheshimu na tunajua itakuwa mechi ngumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata pointi tatu muhimu,” amesesema Matola.