Simba yaja na ‘Its not Over, Kazi Iendelee’

Kuelekea mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy utakaopigwa Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa tumekuja na slogan ya ‘Its Not Over, Kazi Iendelee.’

Slogan hii inatokana na ushindi wa mabao 2-0 tuliopata ugenini dhidi ya Jwaneng wikiendi iliyopita nchini Botswana ambapo pamoja na matokeo hayo lakini bado kazi haijaisha.

Kaimu Msemaji wa klabu, Ally Shatry ‘Chico’ amesema Jwaneng ni timu nzuri na itakuja kwa nia moja ya kutaka kupindua matokeo hivyo tumejipanga kuhakikisha tunawakabili na kupata ushindi.

Chico amesema maandalizi ya mchezo yamekamilika kwa asilimia 90 kikosi kiko kambini na wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo huo.

“Kama kawaida yetu kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa tunakuwa na slogan yetu na safari hii ni IT Is not Over, Kazi Iendelee. Hii ina maana kuwa tumepata ushindi ugenini lakini kuna dakika 90 nyingine Jumapili ambazo tunahitaji kupata ushindi, kazi bado inaendelea,” amesema Chico.

Chico ameongeza kuwa wapinzani wetu Jwaneng tayari wametua nchini jana kimya kimya tayari kwa mchezo huo muhimu.

Viingilio vya mchezo huo ni Sh 5,000 mzunguko lakini ukinunua tiketi uwanjani itakuwa Sh 7,000, VIP B na C Sh 20,000 VIP A Sh 40,000 na Platinum Sh 150,000.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER