Simba yaifuata Azam Nusu Fainali ASFC

Ushindi wa mabao 3-0 tuliopata dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo uliopigwa leo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa umetufanya kutinga Nusu Fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC).

Nahodha John Bocco alitufungia bao la kwanza dakika ya 22 kwa mkwaju wa penati baada ya Bernard Morrison kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Zikiwa zimesalia dakika nne kabla ya kwenda mapumziko Bocco alitufungia bao la pili baada ya kugongwa na mpira uliokuwa umeokolewa na mlinzi wa Dodoma.

Medie Kagere alitupia bao la tatu dakika ya 79 akimalizia pasi ya Morrison muda mfupi baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Bocco.

Kipindi cha pili Kocha Didier Gomes aliwatoa Bocco, Luis Miquissone na Clatous Chama na kuwaingiza Kagere, Erasto Nyoni na Mzamiru Yassin.

Kutokana na matokeo hayo, tutakutana na Azam FC katika mchezo wa nusu fainali utakaopigwa kati ya Juni 25-27 kwenye Uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER