Kikosi chetu cha timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 (U-20) kimeichapa bila huruma Ashanti United bao 3-1 katika Michuano ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) uliopigwa Uwanja wa Karume.
Mchezo ulianza kwa kasi huku tukiliandama lango la Ashanti ambapo ilituchukua dakika 10 kupata bao la kwanza lililofungwa Micheal Godlove.
Kassim Katelego alifunga bao la pili dakika ya 20 baada akimalizia mpira wa kutengwa uliopigwa na Godlove.
Baada ya bao hilo Ashanti walikuja juu na kusawazisha kwa mkwaju wa penati dakika ya 30 kupitia kwa Msheto.
Hamimu Mussa alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga la mwisho kwa shuti kali nje ya 18 dakika ya 35.
Mchezo Unaofata itakuwa dhidi ya Cambiasso Utakaopigwa Januari 24 uwanja wa Karume.
One Response