Simba Queens yatinga nusu fainali kibabe, yaichakaza FAD FC 10-0

Kikosi chetu cha Timu ya Wanawake ya Simba Queens, kimefanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano ya Cecafa Samia Women Cup baada ya kuichakaza bila huruma FAD FC ya Djibouti kwa mabao 10-0 mchezo uliopigwa uwanja wa Moi Kasarani.

Ushindi tuliopata leo unatufanya kutinga moja kwa moja nusu fainali ya michuano hiyo tukifikisha alama saba na kukalia usukani wa kundi A.

Katika mchezo huo tulitawala mchezo kwa dakika zote 90 huku tukionyesha kiwango bora ambacho kila aliyeshuhudia amekubali kuwa tuko vizuri.

Washambuliaji wetu Oppah Clement na Mawete Musolo wamefunga mabao matatu ‘hat trick’ kila mmoja na kuonyesha wazi kuwa hatuna utani linapokuja suala la kuamua mechi.

Asha Djafar na Aisha Juma kila mmoja amefunga mabao mawili na kukamilisha ushindi huo monono kutoka kwa vijana wetu.

Kocha Mkuu Hababuu Ally aliwatoa Zena Khamis, Fatuma Issa na Mawete na kuwaingiza Asha Djafar, Maimuna Khamis na Shelda Boniface.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER