Simba Queens yashusha straika Mkongo

Zikiwa zimebaki siku tatu kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya Wanawake (Serengeti Lite Women’s Premier League) kikosi chetu cha Simba Queens kimeshusha mshambuliaji mahiri kutoka nchini DR Congo.

Mshambuliaji huyo mwenye uwezo mkubwa wa kucheka na nyavu anajulikana kama Pambani Falonne Kuzoya kutoka Timu ya FCF Amani inayoshiriki Ligi ya DR Congo.

Pambani alikuja nchini mwezi uliopita na kikosi cha FCF Amani katika ziara ya siku mbili kwa ajili ya mazoezi ambapo benchi letu la ufundi lililona ubora wake.

Pambani anatagemewa kutengeneza muunganiko mzuri (combination) na nyota Oppah Clement katika idara yetu ya ushambuliaji.

Tayari nyota huyo yuko mazoezini na wenzake kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu wa kwanza dhidi ya Ruvuma Queens utakaopigwa Alhamisi Uwanja wa Mo Simba Arena.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER