Kikosi chetu cha timu ya Wanawake ya Simba Queens kimeshika nafasi ya nne baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Lady Doves ya Uganda katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu wa michuano ya Caf Women’s Champions League Cecafa Qualifiers 2021 uliopigwa Uwanja wa Kasarani.
Mchezo huo haukuwa na kasi sana huku mbinu zaidi zikitumika na mpira ukichezwa zaidi eneo la katikati ya uwanja.
Doves walipata bao la kwanza dakika ya 21 kupitia kwa Nakacwa Spencer aliyepiga shuti kali lililomshinda mlinda mlango wetu Gelwa Yona.
Dakika ya 82 Doves walipata bao la pili lililofungwa na Fazila kufuatia piga nikupige langoni kwetu kabla ya mpira kumkuta mfungaji.
Asha Djafar alitupatia bao letu pekee dakika ya 87 akimalizia pasi ya Aisha Juma baada ya vijana wetu kufanya shambulizi kali langoni mwa Doves.