Simba Queens yaishushia kipigo kizito Alliance Girls

Simba Queens imeendelea kuthibitisha kuwa imedhamiria kwa dhati kutetea taji la ligi ya Wanawake msimu 2024/25 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Alliance Girls katika mchezo uliopigwa katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Tulianza mchezo kwa kasi ambapo ilituchukua dakika nane kupata bao la kwanza lililofungwa na Elizabeth Wambui kwa shuti kali nje ya 18.

Mshambuliaji Jentrix Shikangwa alitupatia bao la pili dakika ya 23 kwa shuti kali la chini chini baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Alliance.

Dakika 10 baadae Esther Mayala alitufungia bao la tatu baada ya kumalizia Mpira wa adhabu uliopigwa na Precious Christopher na kutufanya kwenda mapumziko tukiwa mbele kwa mabao 3-0.

Kipindi cha pili tulirejea kwa kasi ambapo mpira wa mrefu uliopigwa na mlinda mlango Janeth Shija ulimfikia Jentrix ambaye aliwazidi maarifa walinzi wa Alliance na kutufungia bao safi la nne dakika ya 57.

Precious Christopher alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga bao la tano dakika ya 80 na kutuhakikishia alama tatu muhimu ugenini.

Kocha Mkuu Yussif Basigi alifanya mabadiliko ya kuwatoa Ester Mayala, Elizabeth Wambui, Precious Jentrix na Vivian Corazone na kuwaingiza Mary Saiki, Amina Bilal, Ritticia Nabbosa, Shelda Boniface na Mwanahamisi Omary.

Queens imeendelea kujikita kileleni mwa msimamo baada ya kufikisha pointi 25 kufuatia kucheza mechi tisa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER