Simba Queens yaipiga ‘mkono’ The Tiger Queens

Timu yetu ya Simba Queens imeendeleza wimbi la ushindi katika ligi ya Wanawake (Serengeti Lite Women’s Premier League) baada ya kuichakaza bila huruma The Tigers Queens uliopigwa Uwanja Mo Simba Arena.

Tulianza mchezo huo kwa kasi ambapo dakika ya tatu tu Opa Clement alitupatia bao la kwanza kabla ya Sabinah Thom kuongeza la pili dakika ya 17.

Dakika ya 30 Olaiya Barakat aliongeza bao la tatu na kutufanya kwenda mapumziko tukiwa mbele kwa mabao 3-0.

Kipindi cha pili tuliongeza kasi na kuliandama lango la Tigers Sports ambapo dakika ya 85 Asha Ramadhan alitufungia bao la nne kwa shuti kali nje ya 18.

Joelle Bukuru alikamilisha karamu ya mabao baada ya kutupia la tano kwa mpira wa adhabu uliotinga moja kwa moja wavuni dakika ya 90.

Kocha Sebastian Nkoma aliwatoa Olaiya Barakat, Vaileth Machela, lAsha Djafar, Sabinah Thom na kuwaingiza Fallone Pambani, Amina Ramadhani, Jackline Albert na Mercy Tagoe.

Matokeo haya yanatufanya kufikisha pointi 21 baada ya kushinda mechi zote saba tulizocheza hadi sasa.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER