Simba Queens yaichapa JKT Meja Isamuhyo

Simba Queens imerejea kileleni mwa msimamo wa Ligi ya Wanawake Tanzania (TWPL) baada ya kuifunga JKT Tanzania mabao 4-3 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo.

JKT walikuwa wakwanza kupata bao kwa mkwaju wa penati dakika ya 11 kupitia Anastazia Anthony.

Jentrix Shikangwa aliisawazishia Queens bao hilo dakika ya 17 kwa mkwaju wa penati baada ya Janeth Christopher kuunawa mpira ndani ya 18.

Dakika ya 27 Shikangwa alitupatia bao la pili baada ya kuunganisha mpira wa krosi uliopigwa na Asha Djafar.

Kipindi cha pili JKT walirudi kwa kasi na kupata mabao mawili dakika ya 57 na 70 kupitia kwa Donisia Minja na Jamila Rajabu.

Dakika 74 Vivian alitupatia bao la tatu la kusawazisha baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Asha Djafar.

Jentrix alitupatia bao la nne dakika ya 78 baada ya kuunganisha mpira wa krosi uliopigwa na Elizabeth Wambui

Kocha wa Simba Queens alifanya mabadiliko ya ya kumtoa mlinda mlango Janeth Shija na kumuingiza Winfrida Seda.

Ushindi huu umeifanya Queens kufikisha pointi 40 ikiwa juu kwa alama mbili dhidi ya JKT Tanzania.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER