Simba Queens yaendeleza ubabe, yaipiga Oysterbay Girls ‘8 O’clock’

Timu yetu ya Wanawake ya Simba Queens imeendelea kutoa vipigo vikali baada ya kuichakaza bila huruma Oysterbay Girls mabao 8-0 katika mwendelezo wa Serengeti Lite Women’s Premier League mchezo uliopigwa Uwanja wa Mo Simba Arena.

Kama kawaida tulimiliki sehemu kubwa ya mchezo ambapo tulienda mapumziko tukiwa mbele kwa mabao 3-0 yaliyofungwa na Asha Djafar aliyetupia mawili na Opah Clement.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi na kuongeza karamu ya mabao kupitia kwa Aisha Juma aliyefunga mawili, Asha Djafar aliyefunga mawili tena na kukamilisha hat trick, Opah akitupia tena huku la mwisho wakijifunga wenyewe baada ya msako mkali.

Ushindi wa leo unatufanya kufikisha alama sita na mabao 23 katika mechi mbili tukiwa hatujaruhusu bao lolote.

Kocha Sebastian Nkoma aliwaingiza Fatuma Issa, Danai Bhobho naAisha Juma kuchukua nafasi za Zena Khamis, Koku Ally na Jackline Albert.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER