Simba Queens kurejea mazoezini leo kujiandaa na ligi

Timu yetu ya Wanawake ya Simba Queens leo itaanza mazoezi rasmi kujiandaa na Ligi Kuu ‘Serengeti Lite Women’s Premier League’ ambayo inatarajia kuanza Novemba 13.

Simba Queens itaanza mazoezi katika Uwanja wetu wa Mo Simba Arena jioni na kuingia kambini moja kwa moja.

Malengo yetu ya msimu huu ni kuhakikisha tunatetea ubingwa wetu ili kupata nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa ya Wanawake msimu ujao.

Kama tutafanikiwa kutetea ubingwa wetu msimu huu itakuwa tumetwaa taji hili kwa mara tatu mfululizo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER