Simba Queens ipo tayari kwa Dabi Kesho

Kocha Mkuu wa Simba Queens, Yussif Basigi amesema kikosi chake kipo kamili kwa ajili ya mchezo wa Dabi dhidi ya Yanga Princess utakaopigwa kesho saa 10 jioni Uwanja wa KMC Complex katika muendelezo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (TWPL).

Basigi amesema kutokana na ugumu wa ligi ambao umesababisha alama kuwa karibu karibu hivyo kwenye mechi zote zilizosalia tunatakiwa kupata matokeo chanya.

Basigi ameongeza kuwa mchezo wa kesho utakuwa mgumu lakini kikosi chetu kipo tayari kuhakikisha haiwaangushi mashabiki ambao watakuwa wamejitokeza kwa wingi uwanjani.

“Kutokana na ushindani mkubwa uliopo kwenye ligi kwa sasa hakuna nafasi ya kudondosha alama yoyote katika mechi zilizobaki.

Basigi ameendelea kusema kuwa “ni kweli utakuwa mchezo mgumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda na kuwapa furaha Wanasimba.”

Kwa upande wake nahodha wa timu, Violeth Nicholaus amesema wao wapo tayari kupambana hadi mwisho kuhakikisha malengo ya ushindi yanafanikiwa.

“Sisi kama wachezaji tupo tayari kwa ajili ya mchezo. Tunajua itakuwa mechi ngumu ukizingatia ni Dabi lakini tupo kamili na tunaamini tutaibuka na ushindi,” amesema Violeth.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER