Kikosi chetu kitaingia kambini leo baada ya mazoezi ya jioni kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa Novemba katika 19 Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Kikosi kilianza mazoezi wiki moja iliyopita ambapo wachezaji walikuwa wanatokea nyumbani ila leo jioni wataingia kambini moja kwa moja kujiandaa na mtanange huo.
Wachezaji waliokuwa katika kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kilichocheza jana na Madagascar nao ni miongoni mwa watakaoingia kambini.
Nyota wetu watatu, Rally Bwalya, Duncan Nyoni na Peter Banda wao hawataingia kambini leo kutokana na kuwa na majukumu ya timu zao za taifa na wanatarajiwa kutua nchini baada ya kumaliza mechi zao.
Hii itakuwa kambi ya kwanza ya Kocha Mkuu Pablo Franco ambaye ametua nchini siku tano zilizopita tayari kukinoa kikosi chetu.
One Response