Simba kuhamasisha ulipaji Kodi kwa hiari

Uongozi wa klabu umeweka wazi kuwa kuanzia sasa umebeba dhamana ya kuhamasisha ulipaji Kodi wa hiari kupitia michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambayo tumeingia hatua ya nusu Fainali.

Makubaliano hayo yamefanyika baina ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda na Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu Bi. Zubeda Sakuru yaliyofanyika makao makuu ya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam ambapo pia imeichangia Shilingi Milioni 50 ili kufanikisha mchezo wetu wa marudiano dhidi ya Stellenbosch utakaopigwa nchini Afrika Kusini Jumapili ijayo.

Katika mazungumzo yao Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Mwenda amesema michezo inabeba kundi kubwa la watu wa rika na hali tofauti hivyo ni mahala sahihi kutumia majukwaa ya michezo kuhamasisha uhiari katika kulipa Kodi.

“Hakuna ubishi kuwa michezo inakusanya watu wengi kwa wakati mmoja huku soka likiwa ndio kivutio zaidi kwahiyo tunaamini kupitia Klabu ya Simba tutakuwa tumeongeza idadi kubwa ya walipa Kodi,” amesema Bw. Mwenda.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu, Bi. Zubeda ameihakikishia TRA kwamba tutakwenda kuhamasisha ulipaji Kodi wa hiari kwa nguvu zote tukitambua kuwa maendeleo ya michezo nchini yanatokana na ulipaji wa kodi.

“Maendeleo yoyote kwenye nchi yanatoka na ulipaji wa kodi, leo tumeungana na TRA kwa ajili ya kuhamasisha wanachi kulipa kwa hiari na kupitia michuano hii ya Kombe la Shirikisho tunaamini tutawafikia wengi,” amesema Bi. Zubeda.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER