Simba kuanza kuzisaka pointi za Kanda ya Ziwa kwa Mwadui Leo

Kikosi chetu leo saa 10 jioni kitashuka katika Uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga katika kuzisaka alama tisa za Kanda ya Ziwa kwa kuikabili Mwadui FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Mchezo wa leo ni wa kwanza kati ya mitatu ya Kanda ya Ziwa ambapo itafuatiwa na mechi dhidi ya Kagera Sugar na Gwambina.

Kikosi kiliwasili mkoani hapa jana jioni kikitokea jijini Mwanza kilipofanya mazoezi ya mwisho ya kujiweka sawa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kabla ya mtanange wa leo.

Kuelekea mechi hizo tatu benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomez limeamua kuondoka na wachezaji wote 28 waliosajiliwa kwa ajili ya kuhakikisha tunarejea jijini Dar es Salaam tukiwa na alama zote tisa.

Tunaingia kwenye mchezo wa leo tukiwa
na kumbukumbu ya ushindi mnono wa mabao 5-0 tuliopata wiki iliyopita dhidi ya Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na kufanya kufikisha alama 49 tukiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo.

TAARIFA YA KIKOSI

Wachezaji wote 28 waliosafiri wapo kwenye hali nzuri kuelekea mchezo wa leo na hakuna yeyote atakayekosekana kwa ajili ya majeruhi au kutumikia adhabu ya kadi.

Kocha Gomez amesema malengo yetu ni kuhakikisha tunapata ushindi katika mechi zote tatu za Kanda ya Ziwa ili kukaa kileleni kwa msimamo na hatimaye kutetea ubingwa.

MCHEZO WA MZUNGUKO WA KWANZA

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Uhuru, Oktoba 31, 2020 tuliichakaza Mwadui kwa kuifunga mabao 5-0.

Nahodha John Bocco alitufungia mabao mawili huku mengine yakiwekwa kambani na Ibrahim Ajibu, Hassan Dilunga na Said Ndemla.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER