Simba kambini leo kuivutia kasi Yanga

Baada ya mapumziko ya siku moja kikosi chetu leo kinaingia kambini kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga utakaopigwa Jumamosi Septemba 25, saa 11 jioni Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Baada ya kumalizika kwa Tamasha la Simba Day wachezaji walipewa mapumziko ya siku moja kusalimia familia zao kabla ya leo kuingia kambini rasmi.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu, Ezekiel Kamwaga amesema maandalizi ya mchezo yanaendelea vizuri na wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri.

Kamwaga amesema kuelekea mchezo huo hakuna mchezaji atakayekosekana kutokana na majeruhi hivyo benchi la ufundi litakuwa na wigo mpana wa kupanga kikosi.

“Kikubwa nawataka mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi kama kawaida yetu na sisi ndiyo wenyeji wa mchezo, kwa hiyo tunapaswa kuonyesha mfano,” amesema Kamwaga.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER