SIMBA HIYOOO KILELENI, YAICHAKAZA AL AHLY

Kikosi cha Simba leo kimesimama kileleni mwa msimamo wa Kundi A wa Klabu Bingwa Afrika, baada ya kuichapa Al Ahly ambao ndiyo Mabingwa watetezi wa michuano hiyo.

Katika mchezo uliomalizika kwa bao moja bila kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Simba waliutumia vema uwanja wa nyumbani kwa kupata matokeo hayo yaliyoisimika kileleni katika kundi lake.

Bao pekee kwenye mchezo huo, limefungwa na Luis Miquissone dakika ya 31 baada ya kugongeana na Clatous Chama na kuachia shuti la mguu wa kulia lililomshinda mlinda mlango wa Ahly, Mohammed El Shenawy.

Ushindi huo unatufanya kufikisha alama sita baada ya kushinda mechi zote mbili za kwanza huku mchezo wa kwanza tukiwachapa bao moja AS Vita ugenini wiki mbili zilizopita.

Simba tumekuwa timu ya kwanza kuifunga Al Ahly kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika chini ya kocha, Pitso Mosimane baada ya timu hiyo kupata ushindi kwenye michezo sita mfululizo tangu alipochukua kibarua hicho mwaka jana.

Licha ya kupata ushindi huu lakini kikosi chetu kimeonyesha kandanda safi muda wote ukiwafanya mashabiki waliojitokeza uwanjani kulipuka kwa shangwe.

Mchezo wetu unaofuata utakuwa Machi 5 mwaka huu dhidi ya El Mereikh ambapo tutawafuata nchini Sudan.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER