Mchezo wetu Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Coastal Union uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa umemalizika kwa sare ya bila kufungana katika mechi ambayo ilikuwa kali na ya kuvutia.
Mchezo huo ulianza kwa kasi huku tukifika mara nyingi langoni mwa Coastal ambao walicheza kwa kuzuia na kufanya mashambulizi machache ya kushtukiza.
Nyota wetu Sadio Kanoute na Mzamiru Yassin walishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia nakutolewa wote dakika ya 42.
Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi na kuliandama lango la Coastal muda wote lakini changamoto ikawa kubadili mashambulizi kuwa mabao.
Dakika ya 93 mlinzi wetu Henock Inonga Baka alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumpiga kichwa Issa Abushehe wa Coastal.
Kocha Hitimana Thierry aliwatoa Kanoute, Mzamiru, Hassan Dilunga na Mohamed Hussein na kuwaingiza Jonas Mkude, Bernard Morrison, Yusuph Mhilu na Medie Kagere.