Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu Ahmed Ally ameingia katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa staili tofauti kabla ya kuanza kukitambulisha mbele ya mashabiki kikosi chetu tutakachokitumia katika msimu wa 2025/2026.
Ahmed aliingia uwanjani kama kiongozi wa kikosi cha ulinzi na usalama huku akiwa ameambatana na idadi kubwa ya walinzi ikiwa ni tofauti na ilivyokuwa mara zote mbili alizowahi kuingia uwanjani kwa ajili ya kutambulisha wachezaji.
Tumekuwekea picha za matukio mbalimbali wakati Ahmed alivyoingia uwanjani na jinsi alivyokuwa akitambulisha wachezaji.