Sbai Karim Kocha mpya wa viungo

Klabu yetu imefikia makubaliano na Sbai Karim raia wa Tunisia ambaye atakuwa kocha wetu wa viungo na kocha msaidizi.

Sbai atakuwa pamoja na Seleman Matola kwenye kumsaidia Kocha Mkuu Zoran Maki kwenye kutimiza majukumu yake ipasavyo.

Sbai na Kocha Zoran wanafahamiana vizuri  kwani wamefanya kazi pamoja katika Timu za Wydad Casablanca (Morocco), CR Belouzdad (Algeria) Al Hilal (Sudan) na Al Tai (Saudi Arabia) akiwa msaidizi wake.

Sbai ni kocha msomi mwenye leseni ya Daraja A ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF).

Sbai ameifundisha Klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco kuanzia 2017 mpaka 2020 na kufanikiwa kuchukua mataji makubwa ya Afrika.

Msimu wa 2018/19 alicheza mchezo wa CAF Super Cup lakini timu yake ya Wydad ilipoteza mechi.

Msimu wa  2020/2021 alikuwa akiitumikia klabu ya Al Hilal ya Sudan.

Uongozi wa klabu umezingatia uhusiano chanya uliopo baina ya Kocha Zoran na Sbai ambapo tunaamini kufahamiana kwao kutarahisisha muunganiko wa haraka kikosini kuelekea msimu mpya wa ligi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER