Uongozi wa klabu unatangaza kufikia makubaliano ya kumsajili kiungo mkabaji, Hamed Ismael Sawadogo raia wa Burkinafaso.
Kiungo huyu fundi mwenye uwezo wa kukaba na kukaa na mpira mguuni amesaini mkataba wa miaka miwili akitokea Difaa El Jadida ya Morroco.
Sawadogo anatarajia kuwasili nchini kesho Jumapili alfajiri ambapo atasubiri kujiunga na kikosi kitakapowasili Jumanne kutokea Dubai.
Sawadogo anayetumia mguu wa kushoto ana umri wa miaka 26 na amewahi kuzitumikia klabu kadhaa barani Afrika ikiwemo ENPPI ya Misri, US Ouagadougou ya nyumbani kwao Burkinafaso.
Sawadogo anakua mchezaji wa pili kusajiliwa kwenye dirisha hili akitanguliwa na Saido Ntibanzokiza ambaye tayari ameshaanza kazi na amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi.
Usajili wa Sawadogo ambaye anaruhusiwa kucheza hadi mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika si wa mwisho katika dirisha hili tunategemea kabla ya kufungwa nyota wengine watatambulishwa.
Wasifu wa mchezaji
Jina kamili: Hamed Ismael Sawadogo
Tarehe ya Kuzaliwa: Februari 28, 1996
Uraia: Burkinafaso
Umri: miaka 26
Urefu: mita 1.91
Nafasi: Kiungo Mkabaji
Uzito: Kilo 65
Timu: Simba Sports Club