Saleh Karabaka ni Mnyama

Tumekamilisha usajili wa kiungo, Saleh Karabaka kutoka JKU ya Zanzibar kwa mkataba wa miaka mitatu.

Usajili wa Karabaka mwenye umri wa miaka 23 unakuwa wa kwanza katika dirisha hili dogo.

Karabaka tayari amejiunga na timu Visiwani Zanzibar na ataanza kuonekana akiwa na jezi ya Mnyama katika michuano ya Mapinduzi inayoendelea.

Pamoja na uwezo alionao Karabaka jambo jingine lililotuvutia ni umri wake mdogo ambao tunaamini atakuwa msaada mkubwa kwa timu.

Mchezaji chipuki ni hazina yetu kubwa na hakuna sehemu bora ya kumtambulisha zaidi ya aliyozaliwa na kukuza kipaji chake ambayo ni Zanzibar.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER