Kiungo Mshambuliaji Pape Ousmane Sakho, amechaguliwa Mchezaji Bora wa Mashabiki wa mwezi Januari (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month).
Sakho raia wa Senegal amewapiku nyota wenzake wawili Sadio Kanoute na Henock Inonga ambao aliingia nao fainali.
Katika mwezi Januari Sakho amecheza mechi saba akidumu uwanjani dakika 563 na amefunga mabao matatu huku akionyesha kiwango safi.
Kwa ushindi huo Sakho atakabidhiwa fedha taslimu Sh 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium ACP.
Mchanganuo wa kura zilivyopigwa
Pape Sakho – 58.02% (1015)
Henock Inonga – 34.67% (607)
Sadio Kanoute – 7.31% (128)
4 Responses
I love simba
Simba nguvu moja
Shururu
Gufu moja