Kiungo mshambuliaji Pape Ousmane Sakho, amechaguliwa mchezaji bora wa mchezo wetu wa Nusu Fainali ya Michuano ya Mapinduzi dhidi Namungo FC baada ya kuonyesha kiwango safi.
Licha ya kufunga bao la pili na kusababisha la kwanza lililofungwa na Medie Kagere, Sakho alikuwa mwiba mkali kwa walinzi wa Namungo kwa muda wote aliokuwa Uwanjani.
Pamoja na kuonyesha kandanda safi pia Sakho alikuwa anaburudisha mashabiki kwa jinsi alivyokuwa anauchezea mpira kwa madoido.
Sakho amekabidhiwa fedha taslimu Sh 1,000,000 kutoka kwa wadhamini Kampuni ya Bima ya NIC.
2 Responses
Mwaka lazima tuchukue kombe la mapinduzi Na tumejiandaa ipasavyo