Kiungo mshambuliaji Pape Sakho, amekabidhiwa Tuzo yake ya Mchezaji Bora wa Mashabiki wa Januari (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month).
Sakho amepewa tuzo hiyo Makao makuu ya Emirate Aluminium ACP yaliyopo Sinza Madukani jijini Dar es Salaam baada ya kuwashinda Henock Inonga na Sadio Kanoute.
Baada ya kupewa tuzo hiyo Sakho amewashukuru wadhamini Emirate kutokana na kuwapa chachu wachezaji kufanya vizuri ambapo ni faida kwa timu.
“Nawashukuru Emirate kwa kutoa tuzo, hii inaongeza chachu kwetu wachezaji kujituma na kufanya vizuri kuisadia timu. Tuzo imeongeza kitu kikubwa kwangu na kunifanya kuendelea kujitoa kwa ajili ya Simba,” amesema Sakho.
Kwa upande wake Ofisa Habari wa Emirate Aluminium ACP, Issa Maeda amesema mchakato wa kumpata mchezaji bora wa mwezi Januari ulikuwa mgumu kutokana mchuano kuwa mkali jambo linalozidi kuitangaza vizuri kampuni yao.
“Mchakato ulikuwa mkali wa kumpata mchezaji bora na hilo ndilo tulikuwa tunalitaka na Kampuni yetu imetangazika vizuri, tunajivunia kufanya kazi na Simba,” amesema Maeda.
Sakho amekabidhiwa tuzo na fedha taslimu Sh 2,000,000 na wadhamini Emirate Aluminium ACP.
One Response