Nyota watatu wameingia fainali ya kinyang’anyiro cha kutafuta mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Januari (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month).
Nyota hao ni kiungo mshambuliaji Saido Ntibazonkiza na walinzi Shomari Kapombe na Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’.
Takwimu zao za mwezi Januari
Dakika Mechi Mabao Assist
Saido 270 3 2 1
Kapombe 270 3 0 0
Zimbwe Jr 270 3 0 0
Zoezi la kupiga kura litaanza leo saa 10 jioni kupitia tovuti yetu ya www.simbasc.co.tz na litafungwa Februari mosi saa sita usiku.
Mshindi atakabidhiwa pesa taslimu Sh. 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium Profile.
5 Responses
Muda ushafika
muda tayari
Mjona box la kura halipo??
Saido
Sido Ntibanzokiza