Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema tumepoteza nafasi tano za wazi za kufunga katika sare ya 2-2 dhidi ya Power Dynamos ambazo zingetuwezesha kupata ushindi mnono ugenini.
Robertinho amesema kipindi cha pili tulicheza vizuri na kutengeneza nafasi nyingi ambazo hatukuzitumia vizuri.
Hata hivyo Robertinho amewapongeza wachezaji kwa kazi kubwa waliyofanya katika mchezo wa leo licha ya kupata sare.
“Tumecheza vizuri hasa kipindi cha pili, tumetengeneza nafasi nyingi. Tumepoteza nafasi zaidi ya tano za kufunga lakini huu ndio mpira wa miguu tunarudi nyumbani kujipanga,” amesema Robertinho.
Kwa upande wake, mlinzi wa kati Che Fondoh Malone amesema bado tuna nafasi ya kufanya vizuri katika mchezo wa marudiano jijini Dar es Salaam hivyo tunarudi kujipanga.
“Hatujakata tamaa ya kusonga hatua ya makundi, tuna dakika 90 nyingine nyumbani ambazo tunaamini tutazitumia vizuri na kuingia hatua ya makundi,” amesema Che Malone.