Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema amewaelekeza wachezaji kucheza kama ilivyokuwa kipindi cha pili katika mchezo wa African Football League (AFL) dhidi ya Al Ahly uliopigwa Ijumaa Uwanja Benjamin Mkapa.
Robertinho amesema kipindi cha pili tulicheza vizuri katika mchezo wa kwanza tunapaswa kufanya hivyo pia katika mechi ya kesho.
Robertinho amesema maandalizi ya mchezo yamekamilika na tumekuja kwa lengo la kuhakikisha tunashinda na kuvuka nusu fainali.
“Siku zote mimi ni mtu chanya, itakuwa mechi ngumu Al Ahly ni timu kubwa lakini tumejipanga. Kila kitu kinaenda vizuri nawaamini wachezaji wangu tupo tayari kushinda,” amesema Robertinho.
Kwa upande wake kiungo mshambuliaji, Willy Essomba Onana amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri kamili kupambana kuhakikisha tunafikia malengo.
“Tupo tayari kwa mchezo wa kesho, haitakuwa rahisi lakini tumejipanga kuhakikisha tunawapa furaha mashabiki wetu,” amesema Onana.